1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Mapigano yazuka upya kati ya Serikali na Waasi wa Kitamil.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq8

Mapigano yamezuka upya katika kisiwa cha Sri Lanka kati ya jeshi la serikali na waasi wa Kitamil.

Wapiganaji wa chini kwa chini wa Tamil Aelam wanalilaumu jeshi la serikali kwa kuingia na vifaru katika eneo la mashariki lisilomilikiwa na yeyote kwenye jimbo la Batticaloa.

Serikali ya Sri Lanka imekanusha madai ya Watamil, na kusema kuwa waasi hao ndio walioanzisha maafa katika eneo hilo lisilimilikiwa na yeyote.

Mnamo mwaka huu pekee, zaidi ya raia elfu tatu, wanajeshi na waaasi wameuwawa katika mapigano ya kijeshi, na kuyafanya makubaliano ya kusitisha matumizi ya silaha kuingia dosari.