1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Watu 16 wauawa katika shambulio dhidi ya kituo cha wanajeshi wa serikali

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1R

Jeshi la Sri-Lanka limesema kwa uchache watu 16 wameuawa katika shambulio ambalo inadaiwa lilifanywa na waasi wa Tamil Tigers kwenye kituo cha wanajeshi wa majini cha Galle kusini mwa nchi. Mfanyakazi wa meli moja aliuawa pamoja na washambuliaji 15. Wizara ya ulinzi imesema shambulio hilo lilifanywa na watu waliotumia boti la uvuvi.

Hili ndilo shambulio la kwanza kabisa kwenye kituo cha kijeshi katika eneo hilo la kusini mwa nchi. Hali ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika mji huo wa Galle kuhakikisha usalama. Shambulio hilo kwenye kituo cha Galle, limetokea siku mbili baada ya mauaji ya watu zaidi ya 100 wengi wao wafanyakazi wa meli katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mazungumzo ya kusaka amani kati ya serikali ya Sri-Lanka na waasi wa Tamil Tigers yanatarajiwa kuanza tena mjini Geneva-Usuisi mwishoni mwa mwezi huu.