COLOGNE:Ujerumani yaomboleza vifo vya askari wake | Habari za Ulimwengu | DW | 24.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOGNE:Ujerumani yaomboleza vifo vya askari wake

Ujerumani inaomboleza vifo vya askari wake watatu waliyouawa Jumamosi iliyopita huko Afghanistan.

Miili ya wanajeshi hao iliwasili jana mjini Cologne katika uwanja wa ndege wa jeshi, na katika misa ya wakfu baadaye, waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung alisema kuwa wanajeshi hao walikuwa katika kikosi cha ujenzi huko Kunduz.

Amesema kuwa Ujerumani itaisaidia serikali ya Afghanistan kuwapata wauaji wa wanajeshi hao na kuwafikisha mbele ya sheria.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeir, amezitaka Pakistan na Afghanistan kuongeza ushirikiano ambao utasaidia kuwasambaratisha wataliban

Waziri Steinmeir alisema hayo mjini Islamabad baada ya mazungumzo yake na waziri mwenziye wa Pakistan.

Pakistan imekuwa iklaumiwa ya kwamba imeshindwa kudhibiti mpaka wake, ambao unatumiwa na wapiganaji wa Taliban kuingia Afghanistan kufanya hujuma

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com