1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE:Rais Köhler akemea kiburi cha bara ulaya kwa Afrika

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt7

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amekosoa kile alichokiita kiburi cha mataifa ya Ulaya kuelekea bara la Afrika .Akizungumza katika mkutano wa kanisa la Kilutheri mjini Kologne amesema bara la Ulaya lazima lifanye bidii kuondoa fikra za kikoloni.

Matamshi hayo ya Köhler yameungwa mkono na Kansela Angela Merkel akisema nchi za ulaya hazipaswi kujikweza wakati inaposhughulikia suala la Afrika.

Pia amesisitiza umuhimu wa kutimizwa kwa viwango vya kijamii na mazingira duniani kwa ajili ya ulinzi wa raia.

Ameongeza kusema mkutano uliomalizika wa kilele wa G8 mjini Heilligendamm ulikuwa ni moja ya hatua zitakazochukuliwa kuelekea suala la uchumi katika utandawazi.