1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Washabiki wa kanivali wamiminika mitaani

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtp

Nchini Ujerumani,msimu wa kanivali umeanza leo hii,hasa katika miji iliyokuwa kando ya Mto wa Rhein.Washabiki,kwa maelfu wamekusanyika miji ya Cologne,Düsseldorf na Mainz ambayo ni ngóme za sherehe za kanivali.Mwezi wa Februari sherehe hizo zinafikia kilele chake.Wakati huo,watu wenye mavazi ya urembo na magari yaliopambwa huandamana barabarani katika sherehe kubwa.