1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Ujerumani yaomboleza wanajeshi wake.

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBys

Ujerumani inaomboleza vifo vya wanajeshi wake watatu waliouawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa mhanga nchini Afghanistan.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung amesema wanajeshi hao ambao walikuwa kwenye kundi la ukarabati katika mkoa wa Kunduz kaskazini mwa nchi hiyo, walikuwa wakisaidia ujenzi wa Afghanistan mpya.

Wanajeshi hao waliuawa siku ya Jumamosi iliyopita walipotoka kwenye gari la kijeshi kununua friji sokoni.

Kwenye misa ya ukumbusho punde baada ya maiti za wanajeshi hao kuwasili katika uwanja wa ndege wa Cologne, Waziri Franz Josef Jung amesema Ujerumani itawasaidia maafisa wa Afghanistan kuwakamata na kuwashtaki waliohusika.