1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton atamba kwenye uchaguzi wa awali

5 Machi 2008

Bado kibarua ni kigumu kwa wanaogombea wa Demokratic

https://p.dw.com/p/DIE8
Hillary Clinton akihutubia wafuasi wake baada ya ushindi wa OhioPicha: AP

DALLAS,TEXAS

Seneta John McCain ameshinda uteuzi wa kuwa mgombea wa Chama cha Republican katika uchaguzi ujao wa rais Marekani utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu. McCain ameshinda uteuzi huo baada ya kunyakua ushindi katika uchaguzi wa awali kwenye majimbo ya Texas,Ohio,Vermont na Rhode Island dhidi ya mpinzani wake Mike Huckabee ambaye ameshatangaza kujiondoa kwenye kinyanga'nyiro hicho. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Marekani CNN rais Goerge W Bush pia anatazamiwa kutangaza rasmi kumuunga mkono McCain mwenye umri wa miaka 71.

Kwa upande wa chama cha Demokratic hali haitabiriki lakini Seneta wa jimbo la Illinois Barack Obama amepata ushindi kirahisi katika jimbo la Vermont.Katika jimbo la Texas Hillary Clinton ameongoza pia ameshinda kwenye majimbo ya Rhode Island na Ohio pia .Ushindi huo wa Hillary Clinton sasa umeongeza nguvu kampeini zake katika kuendelea kutafuta uteuzi wa kuwa mgombea wa chama hicho.Hata hivyo Obama bado anaongoza kwa idadi ya wajumbe ambao ni muhimu katika kinyanga'nyiro.