1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yasema iko tayari kuusadia Umoja wa Ulaya

Josephat Nyiro Charo15 Februari 2012

Kwenye mkutano kati ya China na Umoja wa Ulaya unaofanyika mjini Beijing, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, ameahidi kuusadia umoja huo kutatua tatizo la madeni bila kutoa maelezo ya kina kuhusu msaada huo.

https://p.dw.com/p/143Qo
BEIJING, Feb. 14, 2012 Chinese Premier Wen Jiabao (C), European Council President Herman Van Rompuy (L), and European Commission President Jose Manuel Barroso (R) meet with reporters after they attended the 14th China-EU summit at the Great Hall of the People in Beijing, capital of China, Feb. 14, 2012 pixel; picture alliance/ZUMA Press
Viongozi wa China na Umoja wa Ulaya wakutanaPicha: picture alliance/ZUMA Press

Zimepita siku 10 tangu Wen Jiabao alipozungumza kuhusu sarafu ya Euro na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, mjini Berlin. Sasa mkuu huyo wa serikali ya China kwa mara nyengine tena ameahidi msaada wake kwa Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na tatizo la madeni katika eneo linalotumia sarafu ya Euro.

"Nia yetu kuusaidia Umoja wa Ulaya kulitatua tatizo la madeni ni thabiti. Tuna imani na Ulaya na sarafu ya Euro. China iko tayari kushiriki zaidi na kwa karibu kufikia makubaliano pamoja na viongozi wa Ulaya."

Lakini kama ilivyokuwa wakati alipokutana na kansela Merkel, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, hakutoa maelezo zaidi. Mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari alizungumzia juu ya ushiriki wa China katika Fuko la fedha la kimataifa au kwenye Mfuko maalumu wa uokozi katika kanda ya Euro.

Rais wa Umoja wa Umoja wa Ulaya, Herman van Rompuy, ameyaeleza mazungumzo na Wen kuwa ya maana na kwamba mashauriano juu ya mzozo wa madeni yataendelezwa.

"Tunaukaribisha mtazamo mzuri na kujitolea kwa uwazi kwa China na waziri mkuu Wen katika suala zima la uthabiti wa kanda ya Euro na Umoja wa Ulaya."

"Hatimaye kitakuwa kibarua cha China kuamua jinsi inavyotaka kuchangia kuleta uthabiti katika eneo linalotumia sarafu ya Euro," ameongeza kusema van Rompuy. Yeye pamoja na rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso, wamemueleza bwana Wen kwa mara nyengine tena kwenye mazungumzo yao kuhusu hatua za Ulaya kuiimarisha kanda ya Euro.

Herman van RompuyFrom left, China's Prime Minister Wen Jiabao, European Council President Herman Van Rompuy and European Commission President Jose Manuel Barroso stand together during an EU China summit at the EU Council building in Brussels on Wednesday, Oct. 6, 2010. The EU and China meet for a formal summit on Wednesday to discuss the trade gap and currency issues. (AP Photo/Virginia Mayo) +++ Bitte nicht für Flash-Galerien verwenden+++
Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, Rais wa Umoja wa Ulaya, Herman van Rompuy, na Jose Manuel BarrosoPicha: AP

"Ujumbe wetu kutoka upande wa Ulaya uko wazi. Tunafanya kinachopaswa kufanywa ili kurejesha tena uaminifu. Na tutafanikiwa"

China na Umoja wa Ulaya zinataka kufikia mkataba wa kuulinda uwekezaji. Herman van Rompuy ametaka China ilegeze sheria zake ili soko la nchi hiyo liweze kufikiwa vizuri zaidi, ulinzi bora wa mali za watu binafsi na kufutwa kwa mfumo wa ulindaji bidhaa katika soko.

Kuhusu suala la haki za binadamu, China iliitilia guu taarifa ya mwisho ya mkutano wa mwaka 2010, lakini safari hii mambo ni tofauti. Haki za binadamu ni mada itakayojumuishwa katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wa Beijing. Hata hivyo, licha ya kutokuwepo mafungamano, kuna haja ya kuendeleza mdahalo na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya haki za binadamu.

Mwandishia: Kirchner, Ruth/Josephat Charo

Mhariri: Saumu Yusuf