1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China kudhibiti ununuzi wa wachezaji ng'ambo

Bruce Amani
16 Januari 2017

China imesema leo kuwa itapunguza idadi ya wachezaji wa kigeni wanaojiunga na timu za lgii kuu ya kandanda nchini humo ili kupunguza gharama kubwa za kuwaleta wachezaji mahiri kutoka ng'ambo

https://p.dw.com/p/2VrqQ
Fußball Suning Commerce übernimmt Inter Mailand
Picha: picture-alliance/dpa/VCG/MAXPPP

Timu katika Super League ya China zitaweza kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi watatu katika mchuano mmoja wakati msimu mpya wa 2017 utaanza mwezi Machi. Hayo ni kwa mujibu wa sheria mpya zilizochapishwa kwenye tovuti ya Shirikisho la Kandanda la China.

China mwezi uliopita ilivunja rekodi ya uhamisho barani Asia kwa mara ya tano katika mwaka mmoja wakati Shanghai SIPG ililipa Chelsea euro milioni 60 kumpata kiungo wa Brazil Oscar. Nayo klabu ya Shanghai Shenhua ilimsajili mshambuliaji nyota wa Agrentina aliyewahi kuzichezea Manchester United na Manchestre City Carlos Tevez na kudaiwa kumfany akuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi duniani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Iddi Ssessanga