1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea yapata ushindi wa kwanza wa msimu

25 Agosti 2015

mshambuliaji wa Uhispania Pedro alifunga bao wakati akiichezea Chelsea ya Uingereza kwa mara ya kwanza na kuisaidia timu yake hiyo mpya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya West Bromwich Albion

https://p.dw.com/p/1GKw0
England Chelsea Meister Jubel
Picha: Reuters/Sibley Livepic

Hizo ni pointi tatu za kwanza kwa mabingwa hao watetezi msimu huu katika michezo mitatu.

Mlinzi wa timu ya taifa ya Uingereza John Terry alitolewa nje kwa kadi nyekundu lakini Chelsea iliweza kung'ang'ania ushindi wake ambao umeiweka timu hiyo pointi tano nyuma ya viongozi wa Premier League Manchester City , ambao wameendelea na wimbi la ushindi kwa kuizaba Everton kwa mabao 2-0 jana Jumapili.

Manchester United ilishikwa shati siku ya Jumamosi kwa kutoka sare tasa na Newcastle , na Leicester City ilitoka sare pia na Tottenham Hotspurs kwa kufungana bao 1-1 na kusogea hadi pointi saba kutokana na michezo mitatu.

Mario Balotelli Liverpool
Mario Balotelli anaelekea AC Milan kwa mkopo kutoka LiverpoolPicha: imago/BPI

Wakati huo huo mshambuliaji matata wa Liverpool Mario Balotelli anaonekana kujiweka tayari kurejea AC Milan baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita . mazungumzo anaendelea na Liverpool kumrejesha kwa mkopo, mkurugenzi mkuu wa Milan Andriano Galliani amenukuliwa akisema.

Real Madrid ilikabwa koo na Sporting Gijon timu iliyopanda daraja msimu huu na kutoka sare bila kufungana katika mchezo wa kwanza wa kocha Rafa Benitez akiwa na wafalme hao wa mjini Madrid , baada ya mabingwa Barcelona kuanza kampeni ya taji la sita katika miaka minane kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Bilbao.

Atletico Madrid , mabingwa wa mwaka 2014, waliishinda timu nyingine iliyopanda daraja , Las palmas kwa bao 1-0 siku ya Jumamosi, wakati valencia pia imeanza kwa kusua sua baada ya kutoka sare bila kufungana na Rayo vallecano.

Mabingwa wa Italia Juventus Turin iliangukia pua kwa kufunga bao 1-0 na Udinese katika mchezo wao wa ufunguzi, kipigo hicho kimemaliza michezo 47 bila kufungwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Verona na makamu bingwa wa mwaka uliopita AS Roma walitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 wakati Fiorentina iliishinda AC Milan kwa mabao 2-0

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman