1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League:Madrid na B.Munich

Ramadhan Ali20 Februari 2007

Timu 16 zinazoania kuingia duru ijayo ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya zinaingia uwanjani jioni hii .Changamoto inayokodolewa macho mno ni kati ya mabingwa wa Ujerumani B.Munich na Real Madrid ya Spain.

https://p.dw.com/p/CHcb

Jioni hii, duru ya kutoana ya champions League –kombe la klabu bingwa barani ulaya- inarudi uwanjani:

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wana miadi na Real Madrid huko Spian wakati Manchester United ya Uingereza, inaumana na Lille ya Ufaransa.Inter Milan ya Itali, inaitembelea nyumbani Celtic ya Scotland.CAF-shirikisho la dimba la Afrika, likiadhimisha mwaka wake wa 50 lamtunza nishani waziri mkuu wa Ethiopia .

Tukianza na changamoto ya jioni hii kati ya Real Madrid ya Spain na Bayern munich ya Ujerumani m jini Madrid, timu zote mbili ziko mashakani.Wakati Bayern Munich imeteleza tena mwishoni mwa wiki ilipokomewa bao 1:0 na Alemaania Aaachen, Real Madrid sio tu imeoondokewa na Ronaldo, inahofia pia kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wake waliokasirika na ingelipendelea leo kuanza nyumbani mwa Bayern Munich.

Uwanja wa Bernabeu Stadium unatazamiwa kusheheni lakini ni mashabiki wachache tu wanaotumai timu yao kutamba.Kocha wao Fabio Capello, anatarajiwa wakati wowote kuwaacha mkono na mashabiki waliwazomea mastadi 2 wa Brazil: Robinho na Emerson, jumamosi pale Real ilipocheza na Real Betis.

Munich ina nafasi pekee msimu huu kukata tiketi yake kwa msimu ujao wa champions league,kwani nyumbani iko patarini ya kutomaliza miongoni mwa timu 3 za kwanza.

Mabingwa wa Ulaya FC Barcelona wakicheza tena na mastadi wao Ronaldinho wa Brazil na Samuel Eto’o wa Kamerun wanapambana kesho na Liverpool wakati wataliana IOnter Milan watakumbana kesho pia na Valencia ya Spian.Mabingwawa Uingereza Chelsea wanakutana kesho na FC Porto ya Ureno.

Ujumbe wa hadhi ya juu wa FIFA-shirikisho la dimba la africa uko Africa kusini kwa ziara ya siku 5 ya kukagua maandalio ya kombe la kwanza la dunia humo nchini na bara la Africa.

Miongoni mwa ujumbe huo ni mkurugenzi wa FIFA anaehusika na mashindano Jim Brown,mkuu wa vyombo vya labari Alain Leiblang mkuu wa kitengo cha kombe la dunia 2010 Afrika kusini, Michael Palmer na Horst Schmidt.wanakagua viwanja na zana kwa kombe la mashirikisho litakalofungua pazia la kombe la dunia 2009.Viwanja 5 vinatengezwa upya na 5 vyengine vinajengwa upya.

Ujumbe wa FIFA ukiwa Afrika Kusini, ule wa CAF ulikuqa jana Addis Ababa,Ethiopia: CAF imemtunza waziri mkuu wa Ethiopia, Males Zenawio nishani ya dhahbu ya shirikisho hilo kwa kazi zake nzuri za kuendeleza dimba la Afrika.

Likiadhimisha jana nusu karne tangu kuasisiwa kwa CAF KARAMU NA HAFLA MAALUMU ilifanyika mjini Addis Ababa jana na kuoneshwa kwenye TV ikiwa sehemu ya maadhimisho ya kutoa nishani kwa viongozi wa nchi zilizoasisi CAF-nazo ni Ethiopia,Misri,Sudan na Africa Kusini.