1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League kuanza Jumanne

17 Septemba 2012

Champions League kutimua vumbi kwa mara ya kwanza msimu huu Jumanne(18.09.2012) Real Madrid baada ya kuanza ligi ya Uhispania,kwa kusua sua,itaonyesha makucha yake dhidi ya Man City katika champions League?

https://p.dw.com/p/16AXd
The final draw for the UEFA Champions League group A, B, C, D, is displayed on an electronic board after the draw, at the Grimaldi Forum, in Monaco, Thursday, Aug. 30, 2012. (Foto:Claude Paris/AP/dapd)
Champions League kuanza kesho Jumanne(18.09.2012)Picha: AP

Eintracht Frankfurt ni timu iliyotia fora mwanzoni mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga hadi sasa. Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu ilishangiria ushindi wake wa tatu katika michezo mitatu ya Bundesliga kwa kuiangusha Hamburg SV kwa mabao 3-2 jana Jumapili.

Hamburg ilibidi kucheza na wachezaji kumi uwanjani baada ya mchezaji wao Petr Jiracek kutolewa kwa kadi nyekundu muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza. kocha Thorsten Fink nae alionyeshwa kadi nyekundu na kuamriwa kukaa katika eneo la watazamaji baada ya kumlalamikia mwamuzi.

Rafael abeba matumaini ya Hamburg

Mchezaji anayebeba matumaini ya SV Hamburg kuiokoa Rafael van der Vaart alionyesha uwezo wake kuwa anaweza kuisaidia timu hiyo kutoka katika ukingo wa kutumbukia katika kina ambacho haitaweza kutoka msimu huu. Baada ya mchezo huo alisema.

"Nafikiri , kwamba tukubali kuwa tumeshindwa tu, nafikiri , ni kutokana na kwamba hakukuwa na hali ya kuaminiana na hali hiyo ilionekana katika dakika 20 za kwanza na ni bahati mbaya sana".

Mlinzi wa kushoto wa Hamburg SV , Marcell Jansen nae amesikitishwa na kipigo hicho kwa kusema.

Hamburg's midfielder Marcell Jansen thanks the fans after a pre-season friendly football match between Hamburger SV and FC Barcelona in Hamburg, northern Germany, on July 24, 2012. FC Barcelona won the match 1-2. AFP PHOTO / CARMEN JASPERSEN (Photo credit should read CARMEN JASPERSEN/AFP/GettyImages)
Marcell Jansen wa Hamburger SVPicha: AFP/Getty Images

"Goli la pili kwa mara nyingine tena mtu anaweza kusema ni goli linalofungwa dhidi ya Hamburg kila mara, na hii inasikitisha sana, kwa kuwa tulipambana sana".

Bamba Anderson (rear) of Eintracht Frankfurt challenges Artjoms Rudnevs of HSV Hamburg during their German first division Bundesliga soccer match in Frankfurt, September 16, 2012. REUTERS/Kai Pfaffenbach (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER GAME. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050
Mpambano kati ya Eintracht Frankfurt - na Hamburg SVPicha: Reuters

Freiburg nayo ikaizamisha TSG Hoffenheim kwa mabao 5-3 jana Jumapili. Hoffenheim hadi sasa haijapata point, baada ya kupata kipigo cha tatu katika michezo mitatu ya Bundesliga msimu huu, na kocha Marcus Babbel yuko katika hatari ya kuwa kocha wa kwanza katika bundesliga msimu huu kibarua kuota majani.

Mabingwa watetezi Borussia Dortmund hawakuwa na shida kuipa kibano Bayer Leverkusen cha mabao 3-0 nyumbani , wakati Bayern Munich imeonyesha misuli yake msimu huu kwa kushinda mchezo wa tatu mfululizo dhidi ya Mainz 05 katika uwanja wake wa nyumbani wa Allianz Arena mjini Munich.

Fußball Bundesliga 3. Spieltag: FC Bayern München - FSV Mainz 05 am Samstag (15.09.2012) in der Allianz Arena in München (Oberbayern). Manuel Neuer (l-r), Bastian Schweinsteiger, Javier Martinez, Xherdan Shaqiri und Claudio Pizarro von München freuen sich über den 3:1-Sieg. Foto: Andreas Gebert dpa/lby (Achtung: Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z.B. via Bilddatenbanken).)
Wachezaji wa FC Bayern München - wakitoka kifua mbele dhidi ya 1. FSV Mainz 05Picha: Reuters

Hannover 96 ikaikaba koo Werder Bremen kwa ushindi wa mabao 3-2, wakati Borussia moenchengladbach ikatolewa jasho na FC Nürberg kwa kulazwa mabao 3-2 pia. Katika mchezo ambao ulikuwa pia na ugeni mzito wa aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Henry Kissinger, Greuther Fürth , timu aliyokuwa akiishabikia waziri huyo wa zamani wa Marekani wakati akiwa mtoto katika mji huo wa Fürth mahali alikozaliwa kabla ya kuhamia Marekani na wazazi wake, kuwapo kwake hakukuweza kusaidia , wakati watoto hao wa nyumbani walipokubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Schalke 04.

Stuttgart iliridhika na sare ya bila kufungana na timu iliyopanda daraja msimu huu ya Fortuna Dusseldorf.

Champions League

Champions league inarejea uwanjani tena kesho Jumanne wakati Real Madrid , moja kati ya timu ambazo zimepata mafanikio makubwa katika mashindano hayo, itakapoikaribisha Manchester City , mabingwa wa Premier League, timu ambayo matumizi yake makubwa katika ununuzi wa wachezaji yameivikisha katika orodha ya vigogo wa soka katika bara la Ulaya kwa sasa.

Mchezo huo wa kundi D unaozikutanisha mabingwa wa ligi ngumu kabisa katika bara la Ulaya hauhitaji kupigiwa upatu zaidi, lakini kocha wa Real , Jose Mourinho tayari kama kawaida yake, ameamsha msisimko kwa matamshi yake kuwa fedha haziwezi kununua mataji ama historia.

Borussia Dortmund's coach Juergen Klopp reacts after the German first division Bundesliga soccer match against Bayer Leverkusen in Dortmund September 15, 2012. Dortmund won the match 3-0. REUTERS/Ina Fassbender (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER GAME. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050
Kocha mkuu wa Borussia Dortmund Jürgen KloppPicha: Reuters

Real itakuwa timu ya kwanza kuweza kushinda michezo yake 100 ya champions league iwapo itafanikiwa kuwadhibiti mabingwa hao wa premier league kesho.

Real imo katika mpambano na Manchester United katika rekodi hiyo , ambapo vigogo hao wa Uingereza wameshinda mara 98 na pia ikifuatiwa na Barcelona ambayo imeshinda michezo 97 katika champions league.

Borussia Dortmund inaikaribisha Ajax Amsterdam katika uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.

Borussia itajaribu kuweka kando msimu uliopita uliokuwa wa fadhaa baada ya kushindwa kutamba katika michezo minne kati ya sita na kumaliza ikiwa mkiani mwa kundi lao. Lakini takwimu zinaonyesha kuwa Borussia imeshinda mchezo mmoja tu kati ya saba dhidi ya timu za Uholanzi na kushindwa kufurukuta kabisa katika michezo mitatu dhidi ya timu hizo ilipocheza nyumbani.

Madrid's coach Jose Mourinho gestures during the Champions League semi-final first leg soccer match between FC Bayern Munich and Real Madrid at the Allianz Arena in Munich, Germany, 17 April 2012. Munich won 2:1. Photo: Andreas Gebert dpa/lby
Kocha wa Real Madrid Jose MourinhoPicha: picture-alliance/dpa

Kinyume chake Ajax imeshindwa katika mchezo mmoja tu dhidi ya timu za Ujerumani katika majaribio tisa.

Mchambuzi wetu wa masuala ya soka , Ramadhan Ali , mhariri wa zamani wa michezo katika DW, anamuunga mkono kocha wa Real Madrid , Jose Mourinho kuwa fedha haziwezi kununua mataji ama historia.

Ni Ramadhan Ali mhariri wa zamani wa michezo wa Idhaa ya Kiswahili DW.

Katika kundi A Dinamo Zagreb inapambana na FC Porto ya Ureno, Montpellier iko nyumbani kupambana na Arsenal London , wakati Olympiakos Pireaus inawakaribisha Schalke 04 ya Ujerumani. Malaga ni wenyeji wa Zenit Saint Petersburg ya Urusi, wakati AC Milan inajaribu bahati yake dhidi ya Anderlecht ya ubelgiji.

Scolari aitupa mkono Palmeiras

Kocha aliyeleta ubingwa wa dunia na timu ya Brazil Luiz Felipe Scolari amevunja ahadi yake ya kuisaidia Palmeiras kupambana dhidi ya kushuka daraja hadi damu ya mwisho, kwa mujibu wa mchezaji wa kati wa club hiyo Jorge valdinia.

Palmeiras ilitangaza wiki iliyopita kuwa Scolari , ambaye aliifunza Brazil na kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2002, ameachana na timu hiyo baada ya kushindwa mara kadha na kujikuta timu hiyo ikiwa katika eneo la kushuka daraja nchini Brazil.

Ameomba kuondoka na ilikuwa ni mshangao mkubwa kwetu, amesema Valdivia kutoka Chile, baada ya Palmeiras kupata kipigo cha mabao 2-0 jana Jumapili dhidi ya Corinthians , ikiwa chini ya kocha mlezi Narciso.

Drogba na Anelka kukosa mshahara?

Huko China mwenyekiti bilionea wa timu ya Shanghai Shenhua amesema kuwa mzozo wa uongozi unaotishia hali ya baadaye ya wachezaji wa kigeni ikiwa ni pamoja na Didier Drogba na Nicolas Anelka haujamalizika. Zhu Jun mfanyabiasha mkubwa ambaye amekuwa akiifadhili timu hiyo kwa miaka mingi na ambaye ametishia kuzuwia mishahara ya wachezaji wa kigeni , amekana kuwa kumekuwapo na makubaliano yoyote.

Anasemekana kuwa anataka washika dau wengine wampe uthibiti mkubwa wa klabu hiyo.

Tennis.

Roger Federer ameendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya wachezaji wa tennis wanaume , katika orodha iliyotolewa leo Jumatatu na shirikisho la mchezo huo duniani. Novak Djokovic anashikilia nafasi ya pili, wakati Andy Murray anaendelea katika nafasi yake ya tatu. Rafael Nadal yuko katika nafasi ya nne.

Kwa upande wa wanawake anayeshikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya wachezaji bora ni victoria Azarenka kutoka Belarus, akifuatiwa na Maria Sharapova wa Urusi katika nafasi ya pili na Agnieszka Radwanska wa Poland yuko katika nafasi ya tatu. Serena William mshindi wa US open wiki iliyopita anashikilia nafasi ya nne.Mjerumani Angelique Kerber yuko katika nafasi ya sita.

Watayarishaji wa mashindano ya Australia open katika mchezo wa tennis wametangaza kuwa michezo ya awali ya taji hilo itafanyika huko nchini China katika hatua ya kuimarisha hadhi ya taji hilo kibiashara. Washindi wa michezo ya Asia wanaume na wanawake watapata kuingia katika mashindano hayo ya Australia open itakayofanyika Januari mwakani.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman.