Chama cha kiliberali FDP chajipatia uongozi mpya | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Chama cha kiliberali FDP chajipatia uongozi mpya

Chama cha -FDP kimejipatia uongozi mpya na kumpokonya wadhifa wake kiongozi wa kundi la chama hicho katika bunge Bibi Birgit Homburger.

default

Usukani wa FDP utaongozwa na Philipp Rösler (kulia) na Rainer Brüderle(kushoto)

Waziri wa uchumi Rainer Brüderle ameteuliwa kuongoza kundi la chama cha FDP katika bunge la shirikisho-Bundestag. Waliberali wanajaribu kujipendekeza tena kwa wapiga kura baada ya kuporomoka chini ya kiwango cha asili mia tano ya kura kufuatia uchambuzi wa maoni ya umma wa hivi karibuni-pigo kubwa ikilinganishwa na asili mia 14 ya kura walizojipatia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.

Uamuzi wa kumpokonya uongozi wa kundi la FDP bungeni mwanasiasa aliyepoteza imani ya wapiga kura wa chama hicho cha kiliberali, Bibi Birgit Homburger, umefuatia miezi kadhaa ya mivutano kati yake na wakuu wenzake chamani.

DOSSIER FDP Personalumstellungen Mai 2011 Teil 2

Mkuu wa zamani na mpya wa kundi la FDP bungeni;R.Brüderle(kulia) na Birgit Homburger

Mvutano ndani ya chama hicho cha kiliberali ndio chanzo cha kuachana waziri wa mambo ya nchi za nje wa serikali kuu, Guido Westerwelle, na wadhifa wake kama mwenyekiti wa FDP mwezi uliopita.

Mabadaliko hayo yamejiri siku chache kabla ya FDP kuitisha mkutano wake mkuu ijumaa ijayo mjini Rostock.

"Hali ni ngumu" amekiri mwenyekiti mpya wa chama cha FDP, Philipp Rösler, mwenye umri wa miaka 38, wakati wa mazungumzo pamoja na waandishi habari mjini Berlin. Ameongeza kusema hata hivyo:

"Ninajua kwa jinsi gani, kwa ushirikiano pamoja na wenzangu chamani, tutakavyoweza kukitoa chama cha FDP katika hali hii ngumu. Na ndio maana ninamshukuru kwa dhati Birgit Homburger, kwa sababu uamuzi wake wa kuachana na wadhifa wake ndio utakaonisaidia kutekeleza fikra niliyo nayo kwa masilahi jumla ya chama cha FDP."

Flash-Galerie Wochenrückschau 2011 KW 16 Silvana Koch-Mehrin Plagiatsvorwürfe

Bibi Silvana Koch-Mehrin

Philipp Rösler, ambae kwa sasa ndie waziri wa afya wa serikali kuu, atakabidhiwa wadhifa wa waziri wa uchumi -na wizara ya afya inatazamiwa kuongozwa na mwanasiasa kijana zaidi, Daniel Bahr, mwenye umri wa miaka 34, mwenyekiti wa FDP katika jimbo la North Rhine Westphalia.

Waliberali wamekumbwa na mkosi mwengine jana baada ya gazeti la mjini Berlin kufichua kwamba chuo kikuu mashuhuri cha Heidelberg kinapanga kumpokonya hadhi udaktari kwa tuhuma za udanganyifu, Silvana Koch-Mehrin, mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika chama hicho cha kiliberali.

Mwandisghi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/afp,dpa

Mhariri: Miraji Othman

 • Tarehe 11.05.2011
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11DaY
 • Tarehe 11.05.2011
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11DaY

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com