1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yasema imewachakaza waasi

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPH

Chad imesema imefaulu kuwaangamiza wafuasi wa kundi la waasi lililohusika kwenye mapigano mashariki mwa nchi hiyo.

Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika eneo hilo kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa muungano wa vikosi vinavyopigania demokrasia na maendeleo, UFDD, tangu mkataba wa kusitisha mapigano ulipovunjika Jumatatu iliyopita.

Waasi hao wamekanusha madai ya serikali wakisema wamewafukuza wanajeshi wa serikali.

Hapo awali waasi wa kundi la UFDD wameuonya Umoja wa Ulaya usimuunge mkono rais wa Chad, Idris Debby, la sivyo watawashambulia wanajeshi wa umoja huo watakaopelekwa katika eneo hilo kuwalinda wakimbizi na kusimamia utoaji wa huduma za kiutu.

Takriban wanajeshi 3,700 wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuwasili katika eneo la mpakani kati ya Chad na Sudan tarehe 31 mwezi ujao.