1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Castro adokeza kuwa atang’atuka.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdAR

Havana.

Kiongozi wa kimapinduzi wa Cuba ambaye ni mgonjwa Fidel Castro amezungumza uwezekano wa kustaafu katika barua iliyosomwa katika televisheni ya taifa ya Cuba jana. Castro , ambaye hajaonekana hadharani kwa muda wa miezi 16, amedokeza kuwa hata rejea madarakani na badala yake ataendelea kuchukua jukumu la kuelekeza kama mzee wa busara, akiishauri serikali ya kikomunist kuhusu masuala muhimu.

Castro kwa muda alitoa madaraka kwa mdogo wake Raul mwezi Julai 2006 baada ya kufanyiwa upasuaji tumboni kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa.