CARACAS: Rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad awasili Nicaragua | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CARACAS: Rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad awasili Nicaragua

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadnejad, amewasili nchini Nicaragua kushauriana na mwenyeji wake, Rais Daniel Ortega.

Rais huyo wa Iran anaizuru Nicragua baada ya kuitembelea Venezuela kwenye ziara yake katika mataifa ya Amerika Kusini.

Rais Mahmoud Ahmedinejad anatarajiwa kuzitembelea Ecuador, na Bolivia, nchi ambazo zinatawaliwa na viongozi wanaoelemea mrengo wa kushoto na ambao ni wapinzani wakubwa wa Marekani.

Nchini Venezuela, Rais Ahmedinejad na mwenzake wa Venezuela, Hugo Chavez wametia saini mikataba kadhaa ya kibiashara na nishati na hivyo kuimarisha ushirikiano wao.

Marais hao pia wameahidiana kuungana mkono katika maswala ya sera za kigeni za mataifa yao.

Ziara hiyo ya rais wa Iran inaonekana kuwa harakati ya kutafuta uungwaji mkono wakati huu ambapo serikali yake inakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutoka Marekani na pia Ulaya kwa sababu ya mradi wake wa nishati ya kinyuklia.

Iran imekuwa ikidai kwamba mradi wake wa nishati ya kinyuklia ni wa amani ilhali wapinzani wake wanasema serikali hiyo ina nia ya kutengeneza silaha za kinyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com