CAPE TOWN:Waziri ataka wanaotaka kuingilia mambo ya Zimbabwe waende Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 21.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAPE TOWN:Waziri ataka wanaotaka kuingilia mambo ya Zimbabwe waende Iraq

Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Trevor Manuel ametetea hatua ya serikali ya nchi hiyo kushughulikia suala la mzozo wa kisiasa nchini Zimbabwe kwa taratibu mno.

Waziri huyo wa fedha wa Afrika Kusini amesema kuwa Wazimbabwe wanatakiwa kuachiwa wenyewe kujiamulia majaaliwa yao bila ya kuingiliwa na watu kutoka nje.

Akizungumza katika mjadala mkali bungeni juu ya suala hilo Trevor Manuel amesema kuwa wale ambao hawaoni umuhimu huo waende Iraq wakaone nini maana ya utawala unapobadilishwa..

Mnamo mwezi March mwaka huu wakuu wan chi za SADC walimteua Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini kusimamia suala la mzozo wa kisiasa nchini Zimababwe lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote wazi zilizoonekana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com