1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN.Hali ya usalama kuimarishwa asema Mbeki

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTj

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini leo ameahidi kuimarisaha mapambano dhidi ya ujambazi na vilevile kupunguza kiwango cha umasiki nchini mwake.

Mbeki aliyasema hayo katika hotuba yake ya mwaka kwa taifa la Afrika Kusini.

Utawala wa rais Mbeki umelaumiwa kwa kuzorota kwa hali ya usalama, rais Mbeki amesema kwamba ataboresha kikosi cha polisi kwa zaidi ya polisi laki moja na elfu themanini katika kipindi cha miaka mitatu na pia kukiimarisha kitengo cha upelelezi.

Amesema serikali yake itapanua mipango ya afya ili kukabiliana na maambukizi ya virusi na ugonjwa wa ukimwi nchini Afrika Kusini.