1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cape Town: ANC chafanya kila liwezekenalo kuepuka mpasuko

7 Desemba 2017

Afisa wa chama tawala nchini Afrika kusini cha African National Congress, ANC amesema chama hicho kinafanya kila  linalowezekana kuepuka mpasuko ndani ya chama

https://p.dw.com/p/2ourV
Süd Afrika ANC-Dissidententreffen in Johannesburg
Picha: AP

Mweka hazina wa chama tawala nchini Afrika kusini cha African National Congress, ANC amesema chama hicho kinafanya kila  linalowezekana kuepuka mpasuko ndani ya chama.

Zweli Mkhize, mgombea katika mchakato wa mbio za kumtafuta kiongozi atakayechukua nafasi ya rais Jacob Zuma kuwa kiongozi  wa chama mwezi huu, amewaambia waandishi habari kwamba ni muhimu wanachama wa ANC wakafanyakazi kujenga umoja badala ya kuendeleza makundi.

Hakuna kiongozi hadi sasa aliyejitokeza kuwa mbele hadi sasa katika kinyang'anyiro hicho, kwa kuwa wanachama wengi wa ANC wanaunga mkono ama makamu wa rais Cyril Ramaphosa ama Dlamini-Zuma katika kuwania uongozi wa ANC.