CAIRO:Kansela Merkel wa Ujerumani amewasili nchini Misri | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO:Kansela Merkel wa Ujerumani amewasili nchini Misri

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewasili Cairo ambako leo jioni atakutana na rais wa Misri,Hosni Mubarak.Misri ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku nne katika Mashariki ya Kati, akijaribu kufufua mazungumzo ya amani yaliokwama. Suala la Lebanon na mgogoro unaohusika na mradi wa kinuklia wa Iran ni masuala yatakayojadiliwa na Kansela Merkel ambae hivi sasa ameshika nyadhifa za urais katika Umoja wa Ulaya na G-8: kundi la nchi nane tajiri zilizoendelea kiviwanda.Ziara ya Merkel itampeleka pia Saudia Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE na Kuwait.Kansela Merkel anafuatana na ujumbe wa kibiashara wa watu 40,ikiwa ni pamoja na waziri wa uchumi wa ujerumani Michael Glos.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com