Cairo. Olmert kukutana na Abbas nchini Misr. | Habari za Ulimwengu | DW | 22.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Cairo. Olmert kukutana na Abbas nchini Misr.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas wanatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo katika mji wa kitalii wa Sharm el –Sheikh nchini Misr.

Mkutano wao huo , ambao utatumika kujadili mzozo wa hivi sasa katika mamlaka ya Palestina , utajumuisha pia rais wa Misr Hosni Mubarak na mfalme Abdullah wa 11 wa Jordan.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza baina ya Olmert na Abbas tangu chama cha Hamas kuyaondoa majeshi ya chama cha Fatah na kuchukua udhibiti wa ukanda wa Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com