1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Misr yaongeza ulizi mpakani.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy0

Misr imeongeza ulinzi katika mpaka wake na ukanda wa Gaza, ikiweka kiasi cha wanajeshi 5,000 baada ya gazeti moja la Israel kusema kuwa Israel inaweza kushambulia kwa mabomu njia za chini ya ardhi zinazotumika kuingiza silaha katika maeneo ya mamlaka ya Wapalestina.

Jeshi la ulinzi limetakiwa kuwalinda raia wa Misr wanaoishi katika mpaka huo.

Gazeti la kila siku la Israel Maariv limeripoti siku ya Ijumaa kuwa mabomu maalum yakuelekezwa yatatumika kuharibu mfumo wa njia za chini ya ardhi unaoshukiwa kuwapo katika eneo hilo.

Jeshi la Israel limekataa kusema lolote kuhusu ripoti hiyo.