1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Magazeti nchini Misr yasitisha uchapishaji.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hf

Magazeti ya vyama vya upinzani nchini Misr yamesitisha uchapishaji leo wakipinga dhidi ya msako wa serikali , ambapo waandishi kadha wamepata kifungo cha muda mrefu jela. Umoja wa waandishi habari nchini Misr umesema kuwa magazeti 23 yanafanya mgomo huo. Hatua hiyo inafuatia kufungwa kwa waandishi saba wa vyombo vya habari mwezi Septema kwa madai ya kusambaza uvumi kuhusiana na afya mbaya ya rais Hosni Mubarak.