1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush sasa yuko Dubai

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coxx

ABU-DHABI:

Rais George W.Bush wa Marekani yuko katika Umoja wa falme za kiarabu UAE akiwa katika kituo cha tatu cha zaira yake ya mashariki ya Kati.Bush amelakiwa na kiongozi wake Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahayan na makamu wake na kiongozi wa Dubai-Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum.Rais Bush anatarajiwa kusifu juhudi za nchi hiyo kuelekea demokrasia hatua kwa hatua.Nchi hiyo ilioko katika Ghuba la Uajemi imekuwa ikitawaliwa na ukoo.Hata hivyo huenda pia akaihakikishia kuwa hataki kukabiliana na Iran ambayo ni jirani wa Umoja wa Falme za Kiarabu-.Kutoka huko Bush ataeleka Saudi Arabia na kukamilisha ziara yake ya siku nane katika mshariki ya kati kwa kwenda Misri.