1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush na Putin waendelea na mazungumzo

3 Julai 2007

Rais George W. Bush wa Marekani na mgeni wake rais Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana kushirikiana katika kutatua mgogoro wa nyuklia wa Iran lakini wameshindwa kuafikiana juu ya suala la makombora ya kujihami.

https://p.dw.com/p/CHBi
Marais W Putin na G.W.Bush
Marais W Putin na G.W.BushPicha: AP

Rais Bush na rais Vladimir Putin anaefanya ziara nchini Marekani wamewaambia waandishi habari baada ya mazungumzo yao Kennenbunkport Maine kwamba wamekubaliana kuwasilisha ujumbe wenye nguvu kwa Iran dhidi ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

Bush amesema wametumia muda mrefu kuzungumzia juu ya suala hilo . Rais huyo ameeleza wasi wasi juu ya mipango ya Iran ya kuendeleza tekinolojia ya kuiwezesha nchi hiyo kuunda silaha za nyuklia.

Lakini Bush na mgeni wake hawakuweza kuafikiana juu ya ulinzi wa makombora barani Ulaya.

Marekani inakusudia kuweka makombora ya kujihami nchini Chek na Poland . Lakini mpango huo unapingwa na Urusi .

Rais Putin aliwaambia wandishi habari baada ya mazungumzo yake na rais Bush kwamba ameitaka Marekani ighairi mpango huo na badala yake ikubali pendekezo la Urusi juu ya kuweka ulinzi huo nchini Azerbaijan.

AM.