1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga:Dortmund yavutwa shati na Hamburg

Aboubakary Jumaa Liongo/ZPR/Reuters10 Aprili 2011

Vinara wa Bundesliga Borussia Dortmund wamenusurika kipigo pale waliposawazisha bao katika dakika za majeruhi dhidi ya Hamburg na kufanya mpambano kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

https://p.dw.com/p/10qjI
Mshambuliaji wa SV Hamburg Ruud van Nistelrooy akishangilia bao dhidi ya Borussia DortmundPicha: AP

Ruud van Nistelrooy aliipatia SV Hamburg bao katika kipindi cha kwanza kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya beki wa Dortmund Mats Hummels kumkwatua Mladen Petric ndani ya box.

Dortmund sasa iko kileleni kwa pointi nane zaidi ya Bayer Leverkusen inayopambana Jumapili hii na St Pauli.Iwapo Leverkusen itashinda basi mwanya wa uongozi utapungua hadi pointi tano.Mechi nyingine itakuwa ni kati ya Borussia Moenchengladbach na FC Cologne:

Fussball, 1. Bundesliga Saison 2010 11 29. Spieltag 1. FC Nuernberg FC Bayern Muenchen easyCredit Stadion Nuernberg
Thomas Muller akiifungia Bayern bao dhidi ya FC NürnbergPicha: picture-alliances/dpa

Wakati huo huo mabingwa watetezi Bayern Munich walilazimishwa kugawana pointi na Nüremberg, mjini Munich kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi iliyoshuhudia mshambuliaji wake Arjen Robben akilimwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo.Bayern wameshushwa sasa kutoka katika nafasi ya tatu na Hannover 96 ambayo iliichapa Mainz mabao 2-0.

Schalke 04 ikiwa nyumbani ililazimika kusubiri hadi katika dakika ya 76 pale Jurado alipoipatia bao pekee la ushindi dhidi ya timu inayofundishwa na kocha wake wa zamani Felix Magath, Wolfsburg.

Kipigo hicho kimedizi kuididimiza zaidi Wolfsburg katika shimo la kushuka daraja, ikiwa na pointi 28 katika nafasi ya tatu kutoka mkiani.Nayo Kaiserslautern iliifunga Stuttgart mabao 4-2

Mabao ya Julian Schuster 2, Papiss Cisse na Heiko Butscher yaliipatia ushindi Freiburg wa mabao 3-2 dhidi ya Hoffenheim.Hapo siku ya Ijumaa Eintracht Frankfurt ilitoka sare ya bao 1-1 na Werder Bremen.

Mwandishi:Aboubakary Liongo