1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga yajindaa kurejea uwanjani

17 Januari 2014

Wakati ligi ya Ujerumani bado iko mapumzikoni na timu zikijiandaa kurejea tena viwanjani wiki ijayo, Ligi ya Uingereza , Uhispania , Italia na Ufaransa zinaendelea

https://p.dw.com/p/1Ast7
Fußball Bundesliga 17. Spieltag Borussia Dortmund gegen Hertha BSC
Borussia DortmundPicha: picture-alliance/dpa

Katika Premier League Chelsea itaumana na Manchester United kesho Jumapili(19.01.2014), wakati Arsenal London inaikaribisha Fulham katika uwanja wa Emiretes jioni ya leo(18.01.2014).

Vilabu vya soka katika ligi ya Ujerumani Bundesliga vinajiandaa kuingia katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo kuanzia Ijumaa ijayo, ambapo timu mbali mbali zimekuwa zikifanya maandalizi kwa kufanya mazowezi ya nguvu pamoja na michezo ya majaribio.

Makamu bingwa wa ligi ya Ujerumani Borussia Dortmund iko kambini mjini La Manga katika siku yake ya 7 ya mazowezi na itaingia uwanjani jioni ya leo kupambana na timu ya daraja la pili ya Kaisersleutern katika mchezo wa majaribio. Mabingwa wa Bundesliga, na Champions League Bayern Munich wako nchini Qatar wakijiandaa kwa mzunguko huo wa pili pamoja na Schalke 04.

Sergio Aguero
Sergio AgueroPicha: AP

Katika ligi ya Uingereza , Premeir League , mshambuliaji hatari wa Manchester City Sergio Aguero atatumia pambano la leo Jumamosi dhidi ya Cardif City kuangalia iwapo maumivu aliyoyapata yameondoka wakati mshambuliaji huyo raia wa Argentina akielekeza macho yake katika pambano la mabingwa wa Ulaya Champions League dhidi ya Barcelona.

Aguero amepachika bao aliporejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa michezo minane akiwa na maumivu ya paja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Blackburn katika duru ya tatu ya kombe la FA siku ya Jumatano.

Nae kocha wa viongozi wa ligi ya Uingereza Premier League Arsenal London, Arsene Wenger ana imani kuwa hazina kubwa aliyonayo ya wachezaji wa kiungo itakiweka kikosi chake juu ya ligi hiyo.

Arsene Wenger, Coach von Arsenal London
Aserne WengerPicha: AP

Arsenal wanaongoza kwa point moja dhidi ya Manchester City iliyoko katika nafasi ya pili wakati wakijitayarisha kuwakaribisha Fulham katika uwanja wa Emirates leo jioni.

Sturridge

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anaamini kuwa Daniel Sturridge anaweza kuongeza kiwango chake cha soka wakati wekundu hao wanaowania ubingwa wa premeier league msimu huu wakiwakaribisha Aston Villa leo Jumamosi.

Sturridge amekuwa nje ya uwanja tangu mwishoni mwa Novemba akiuguza kifundo cha mguu lakini aliingia uwanjani na kupachika bao na kutayarisha lingine katika ushindi wa Liverpool wa mabao 5-3 dhidi ya Stoke City mwishoni mwa juma lililopita.

Na katika ligi ya Uhispania La Liga Real Madrid imeanza kutoa mbinyo mkali katika ligi hiyo dhidi ya viongozi wa ligi Barcelona na Atletico Madrid kwa kusogea karibu katika uongozi wa ligi hiyo kwa ushindi dhidi ya Real Betis siku ya Jumamosi.

Timu zote tatu zinacheza katika harusi tatu katika soka la Uhispania wakati zilipoingia katika awamu ya robo fainali katika kombe la Copa del Rey katikati ya wiki kabla ya kurejea katika michuano ya Champions League mwezi ujao.

Paris St Germain , mabingwa wa ligi ya Ufaransa na viongozi wa sasa wa ligi hiyo wanataka kusisitiza uwezo wao dhidi ya timu zote za Ligue 1 kwa ushindi kesho dhidi ya wageni wao Nantes katika uwanja wa Parc des Princes.

Fußball-Spieler Clarence Seedorf vom brasilianischen Fußballverein Botafogo
Clarence SeedorfPicha: Getty Images

Clarence Seedorf

Na huko Italia mchezaji aliyetawaza mara kadha bingwa wa Champions League akiwa na AC Milan Clarence Seedorf anaanza awamu mpya ya kibarua katika klabu hiyo , mara hii akiwa kocha mlezi , wakati dunia ikiangalia wakati kikosi hicho cha Rossoneri kikiikaribisha Verona kesho Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre

Mhariri: Josephat Charo