1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga "der Klassiker" Dortmund Kuikabili Bayern

23 Novemba 2013

Michezo ya timu za taifa imemalizika sasa ligi zinaanza tena rasmi barani Ulaya. Borussia Dortmund yaikabili Bayern wakati kikosi chake kimesheheni majeruhi katika mchezo muhimu wa "der Klassiker" katika Bundesliga.

https://p.dw.com/p/1AMnw
DORTMUND, GERMANY - NOVEMBER 01: Sokratis (C) of Dortmund celebrates after scoring his team's first goal with team mates during the Bundesliga match between Borussia Dortmund and VfB Stuttgart at Signal Iduna Park on November 1, 2013 in Dortmund, Germany. (Photo by Sascha Steinbach/Bongarts/Getty Images)
Kikosi cha Borussia DortmundPicha: Getty Images

Barcelona ambayo imeelemewa pia na majeruhi huenda ikawakosa wachezaji saba wa timu ya kwanza wakati wakijaribu kuimarisha nafasi yao ya uongozi katika ligi ya Uhispania, La Liga.

Ligi ya Ujerumani Bundesliga inarejea uwanjani leo, lakini mara hii ikiwa na hali nyingine ya mvuto hususan kwa upande wa Bayern Munich na Borussia Dortmund . Timu hizo zinakutana katika mchezo wa 13 wa Bundesliga leo jioni katika uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund zikiwa na kiwango kikubwa cha majeruhi katika kila upande.

FILE - Borussia Dortmund's trainer Juergen Klopp gestures during the UEFA Champions League match Napoli vs Borussia Dortmund at San Paolo stadium, Naples, Italy, 18 September 2013. EPA/CIRO FUSCO (Recropped version - Best quality available - zu dpa 0319 vom 24.09.2013) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kocha wa Dortmund Jürgen KloppPicha: picture-alliance/dpa

Lakini walioathirika zaidi ni Borussia Dortmund ambayo inaogelea katika jinamizi la majeruhi baada ya michezo ya timu ya taifa.

Bayern mbali ya kumkosa nahodha msaidizi Bastian Schweinsteiger, lakini pia haitapata huduma ya winga hatari Frank Ribery.

Munich players Franck Ribery, front, and his teammate Luca Toni, left, celebrate after his penalty kick during the German first division Bundesliga soccer match between FC Bayern Munich and VfL Bochum in Munich, southern Germany, on Sunday, April 6, 2008. (AP Photo/Christof Stache) ** Eds note German spelling of Munich is Muenchen. ** NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS **
Frank Ribery, wa Bayern MunichPicha: AP

Mchezaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuvushwa taji la mchezaji bora duniani amevunjika mbavu katika mchezo wa mtoano wa kuwania tikiti ya kucheza katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil dhidi ya Ukraine, ambapo Ufaransa ilifanikiwa kukata tikiti hiyo.

Mvi zamuota Klopp

Kocha wa BVB , Borussia , Jürgen Klopp anakosa karibu mstari mzima wa walinzi katika timu yake. Mbali ya Neven Subotic , pia atamkosa Mats Hummels na mlinzi wa pembeni Marcel Schmelzer . Kocha wa BVB amesema kuwa ni hali inayomchanganya sana , na kwamba asilimia 80 ya mvi katika nywele zake amezipata wiki hii. Hata hivyo anapaswa kujenga kikosi ambacho kitaikabili Bayern Munich ambayo katika misimu miwili sasa imefikisha michezo 37 bila ya kushindwa na inaongoza Bundesliga kwa points 4 ikiitangulia Borussia Dortmund na Byer Leverkusen.

Ikiwa Bayern itashinda katika mchezo huo unaofahamika hapa Ujerumani kama "der Klassiker", itaipita Borussia kwa points saba. Huenda pengo lisiwe kubwa bado na kubakia katika points 4 iwapo Bayer Leverkusen itapata ushindi dhidi ya Hertha BSC Berlin . Pambano jingine ni kati ya FC Nürnberg ikiumana na VFL Wolfsburg, wakati Eintracht Frankfurt ina miadi na Schalke 04. Augsburg inakumbana na Hoffenheim , wakati Eintracht Braunschweig inatiana kifuani na SC Freiburg timu zote zikiwa mkiani mwa ligi hiyo. Jumapili itakuwa zamu ya Hamburg SV dhidi ya Hannover na Werder Bremen itakuwa mwenyeji wa FSV Mainz 05.

Majeruhi Barcelona

FC Barcelona ambayo nayo imekubwa na balaa la majeruhi katika kikosi chake inaweza kuwakosa wachezaji saba wa timu ya kwanza wakati wakijaribu kujiimarisha katika nafasi yao ya uongozi katika ligi ya Uhispania , La Liga ikiikaribisha Granada leo jioni. Barcelona itamkosa Lionel Messi katika michezo nane katika mashindano matatu kabla ya Krismass baada ya kuumia paja katika mchezo wa mwisho wa Barca dhidi ya Real Betis wiki mbili zilizopita.

Lionel Messi of Argentina's national soccer team waits on the sidelines during their 2014 World Cup qualifying soccer match against Colombia in Buenos Aires, June 7, 2013. REUTERS/Marcos Brindicci (ARGENTINA - Tags: SPORT SOCCER)
Lionel Messi wa BarcelonaPicha: Reuters

Huko nchini Uingereza katika Premier League Arsenal London inakutana na Southampton, Everton ina ikaribisha nyumbani Liverpool, Fulham ina kibarua dhidi ya Swansea, Hull City iko nyumbani ikiisubiri Crystal Palace. Newcastle inapimana nguvu na Norwich, Stoke City inapimana ubavu na Sunderland na West Ham inaikaribisha Chelsea.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae

Mhariri: Yusuf Saumu