1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUCHAREST : Waromania wagoma kumshtaki rais

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0U

Matokeo ya awali ya kura ya maoni nchini Romania yameonyesha kwamba wapiga kura watatu kati ya wanne wameukataa mpango wa bunge wa kumshtaki Rais Traian Basescu ambaye amekuwa akiongoza harakati za kupiga vita rushwa nchini humo.

Bunge lilimsimamisha kazi rais huyo mwezi uliopita baada ya vyama tawala na vile vya upinzani vikiongozwa na Waziri Mkuu Calin Tariceanu kumshutumu Basescu kwa kupindukia madaraka yake ya kikatiba.Matokeo rasmi ya kura hiyo ya maoni iliopigwa jana miongoni mwa Waromania milioni 18 yanatazamiwa kutolewa hapo Jumatatu.

Tokea Romania ijiunge na Umoja wa Ulaya hapo mwezi wa Januari wanadiplomasia wamekuwa wakisema Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imekuwa na wasi wasi kutokana na kuzorota kwa hatua za nchi hiyo kupambana na rushwa iliokithiri.