BUCHAREST: Kura ya maoni yamuunga mkono Basescu | Habari za Ulimwengu | DW | 20.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUCHAREST: Kura ya maoni yamuunga mkono Basescu

Rais wa Rumania Traian Basescu anaetaka kufanya mageuzi nchini,anaweza kubakia madarakani.Matokeo ya mwanzo ya kura ya maoni iliyopigwa siku ya Jumamosi nchini Rumania yameonyesha kuwa kama asilimia 75 ya wapiga kura wamepinga mpango wa bunge wa kutaka kumuondosha madarakani Rais Basescu.Bunge hilo,tarehe 19 mwezi wa Aprili lilimuachisha kazi kwa muda rais Basescu kwa mashtaka ya kukiuka katiba ya nchi na kutumia huduma za idara ya upelelezi kuwachunguza wabunge.Rais Basescu lakini amekanusha madai hayo na amesema,maadui wake wanajaribu kuzuia juhudi zake za kupiga vita rushwa.Matokeo rasmi ya kura hiyo ya maoni yanatazamiwa kutangazwa siku ya Jumatatu.Tangu Rumania kujiunga na Umoja wa Ulaya hapo mwezi wa Januari,wanadiplomasia wamekuwa wakisema kuwa Halmashauri ya Ulaya ina wasiwasi kuhusika na kuzorota kwa hatua za kupiga vita rushwa iliokithiri nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com