1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUCHAREST: Kura ya maoni kuamua hatima ya Basescu

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0c

Wapiga kura nchini Rumania hii leo wamepiga kura ya maoni kuamua hatima ya rais Traian Basescu. Kiongozi huyo ameshtakiwa kwenda kinyume na katiba na hapo tarehe 19 mwezi Aprili,bunge lilimuachisha kazi kwa muda.Basescu,ametuhumiwa na upande wa upinzani kuwa alitumia huduma za idara ya upelelezi,kuwapeleleza wanasiasa mashuhuri.Rais Basescu lakini anadai kuwa maadui wake,wanajaribu kuzuia operesheni yake ya kupiga vita ulajirushwa nchini humo.