1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Mkakati wa kudhibiti uhamiaji usio halali barani Ulaya

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnz

Halmashauri ya Ulaya inataka kuzalisha nafasi za kazi katika nchi za Kiafrika ili kuweza kudhibiti mmiminiko wa watu wanaohamia Ulaya.Waziri wa sheria wa Umoja wa nchi za Ulaya,Franco Frattini amesema,Euro milioni 40 zitawekwa kwa ajili ya awamu ya mwanzo ya mradi huo.Msaada wa fedha,hasa unapaswa kutolewa kwa nchi za Afrika ya Magharibi aliongezea Frattini.Kwa njia hiyo,Umoja wa Ulaya unataka kushughulikia ukosefu wa ajira,jambo linalowafanya Waafrika wengi kuhamia Ulaya.Wakati huo huo,Umoja wa Ulaya utajaribu kudhibiti bora zaidi utaratibu wa kushughulikia uhamiaji wa halali.Frattini ameshauri viwepo vituo vya uhamiaji ambako wahamiaji wa siku zijazo wanaotafuta kazi nchi za Ulaya wataweza kupewa msaada.