BRUSSELS: Wawakilishi wa UM kujadili hali ya baadae ya Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 25.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Wawakilishi wa UM kujadili hali ya baadae ya Kosovo

Kundi la wawakilishi kutoka baraza la usalama la umoja wa mataifa liko mjini Brussels, Ubelgiji kujadili mkakati wa hali ya baadaye ya Kosovo.

Kundi hilo pia litasafiri hadi Kosovo, Belgrade na Vienna licha ya kuwepo upinzani kuhusu uhuru wa Kosovo.

Umoja wa Ulaya na Marekani zinaunga mkono pendekezo la mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Martti Ahtisari kuhusu uhuru wa Kosovo lakini chini ya uangalizi wa jamii ya kimataifa pendekezo hilo linapingwa na Urusi.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatazamiwa kulipigia kura pendekezo hilo.

Kosovo imekuwa chini ya umoja wa mataifa tangu mwaka 1999.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com