BRUSSELS : Urusi yasita kushiriki mkataba wa silaha Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS : Urusi yasita kushiriki mkataba wa silaha Ulaya

Bunge la Umoja wa Ulaya mjini Brussels limeelezea wasi wasi wake juu ya kura ya kauli moja ya bunge la Urusi kusitisha ushiriki wa Urusi katika mkataba muhimu wa udhibiti wa silaha barani Ulaya.

Uamuzi huo wa bunge la Urusi Duma kuhusu agizo lililotolewa na Rais Vladimir Putin hapo mwezi wa Julai unaonekana kuwa ni kujibu mapigo ya mipango ya Marekani kuweka makombora ya kinga nchini Poland na Jamhuri ya Czeck.Mkataba huo wa Majeshi ya Kawaida Barani Ulaya umetiwa saini na nchi 16 wanachama wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa Magharibi NATO na nchi sita wanachama wa zamani wa Mkataba wa Warsaw wa mwaka 1990.

Mkataba huo unaweka viwango vya mwisho kabisa vya akiba ya silaha za kawaida katika eneo kuanzia milima ya Ural ya Urusi hadi mwambao wa bahari ya Atlantiki ya Ulaya ya Magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com