1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wanatumai serikali mpya ya Belgrade itaegemea Ulaya

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYc

Licha ya chama chenye siasa kali kushinda uchaguzi nchini Serbia, mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanasema wanatarajia kuundwa kwa serikali itakayoegemea Ulaya mjini Belgrade.

Chama cha wazalendo kilishinda asilimia 28 ya kura lakini kikashindwa kupata wingi wa kura kuweza kuunda serikali. Sasa chama hicho kinalazimika kutafuta washirika wa kuunda serikali ya mseto.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri mkuu wa jimbo la Kosovo, Agim Ceku, ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa ifanye haraka kuamua hali ya baadaye ya Kosovo. Aidha kiongozi huyo amesema uhuru wa Kosovo ni jambo linalowezekana na lazima lifanyike kwa haraka.

´Sasa kwa kuwa uchaguzi umefanyika tunaweza kufanya haraka kufikia uamuzi juu ya hatima ya jimbo la Kosovo. Na tuna matumaini kwamba jamii ya kimataifa hivi karibuni baada ya uchaguzi huu itatambua kwamba Kosovo iko huru.´

Waziri mkuu Agim Ceku ameyasema hayo baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani nchini Serbia.