1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya kuzungumza tena na Iran

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSy

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamejiandaa kuzidi kuishinikiza Iran juu ya mpango wake wa nuklea wakati wa mkutano wa kila mwezi mjini Brussels leo hii.

Mawaziri hao 27 wanatazamiwa kuahidi kutekeleza vilivyo vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran jambo ambalo kimsingi tayari limekubaliwa hapo mwezi wa Januari.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana amesema anataka kuendeleza mawasiliano na Iran juu ya mpango wake huo wa nuklea uliozusha utata baada ya kuwa na mkutano mpya na msuluhishi mkuu wa masuala ya nuklea wa Iran ambao ameuelezea kuwa wa tija.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir pia alikuwa na kauli kama hiyo ya kuhimiza mazungumzo na Iran kwa lengo la kuleta tija.

Wanadiplomasi wamesema watapinga shinikizo la Marekani na Uingereza kuchukuwa hatua zaidi dhidi ya Iran kwa hivi sasa.

Mwaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika mkutano huo wa Brussels pia wanatazamiwa kuunga mkono mpango wa Marti Ahtisaari kwa ajili ya Kosovo jimbo la Serbia.Mpango huo unataka kutowa uhuru wa kiasi fulani kwa jimbo hilo.