1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya yataka vikwazo kamili dhidi ya Iran

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYj

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wameamuwa kutekeleza kikamilifu vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kwa sababu ya kugoma kwake kusitisha urutubishaji wa uranium.

Mawaziri hao wanaokutana mjini Brussels wamekubaliana kuzuwiya mali za nchi hiyo na kuweka vikwazo vya safari kwa maafisa wa serikali wanaohusika na mpango wa nuklea wa Iran pamoja na kusitisha biashara ya bidhaa zinazohusiana na nuklea. Iran imesema haitowaruhusu kuingia nchini Iran wakaguzi 38 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu ambao walikuwa wanatarajiwa kuitembelea nchi hiyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la vikwazo hivyo hapo tarehe 23 mwezi wa Desemba na iliipa Iran siku 60 kutimiza madai ya azimio hilo.

Iran inaendelea kusisitiza kwamba mpango wa nuklea ni kwa ajili ya kuzalisha umeme tu wakati Marekani na Umoja wa Ulaya zinahofu kwamba inaweza ikawa inajaribu kutengeneza silaha za nuklea.

Wiki iliopita Iran imesema ilikuwa tayari kuweka mashinepewa 3,000 katika mpango wake huo wa nuklea.