1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Ulaya yashauriwa kuwakubali wahamiaji wa muda.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3C

Kamishna wa masuala ya sheria wa umoja wa Ulaya Franco Frattini ameshauri kuwa mataifa ya umoja huo yakubali wahamiaji zaidi wa muda mfupi kutoka Afrika na mataifa ya ulaya mashariki ili kupunguza hali ya idadi kubwa ya wazee katika mataifa ya umoja huo.

Uhamiaji wa aina hiyo , ameongeza , watahitajika kurejea nyumbani baada ya kipindi fulani. Frattini ameuambia mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani na ujumuisho katika mji wa Potsdam nchini Ujerumani kuwa ofisi yake inafanyakazi kuandaa mpango huo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema mataifa mengi ya umoja wa Ulaya yamekuwa na matatizo kama hayo ya kuwajumuisha wahamiaji katika jamii zao.

Wahamiaji milioni 40 wanaishi katika umoja wa Ulaya. Nia ya mkutano huo wa siku tatu ni kuimarisha juhudi za ujumuisho katika bara la Ulaya.