1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya yadai kikosi mchanganyiko Dafur

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYm
Jenerali Parves Musharaf rais wa Pakistan
Jenerali Parves Musharaf rais wa PakistanPicha: PA/dpa

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wameitaka serikali ya Sudan iruhusu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuingia kwenye jimbo la Dafur lenye machafuko ya umwagaji damu ikiwa ni sehemu ya kikosi mchanganyiko na kile la Umoja wa Afrika.

Hata hivyo mawaziri hao wameshindwa kutowa fedha za ziada za Umoja wa Ulaya kukigharimia kikosi chenye zana dhaifu cha Umoja wa Afrika kiliopo hivi sasa huko Dafur.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu mjini Brussels Ubelgiji yameutaka Umoja wa Ulaya kuitishia serikali ya Sudna na vikwazo kwa kuyalenga mapato yake ya mafuta.

Mzozo wa Dafur uliodumu kwa miaka minne inakadiriwa kuuwa watu 200,000 na kuwapotezea makaazi wengine milioni mbili na nusu.