1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Mustakbali wa kisiasa mashakani

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWb

Mustakbali wa kisiasa nchini Ubelgiji uko mashakani kutokana na chama kikubwa kabisa kutangaza kuwa kimeshindwa kuunda serikali ya mseto miezi miwili baada ya uchaguzi mkuu.

Yves Leterme mkuu wa chama cha Waflemish cha Christian Demokratik ameomba aondolewe majukumu ya kuunda serikali baada ya mazungumzo ya dharura ya dakika za mwisho na wanaoweza kuwa washirika wa serikali ya mseto Wakiliberali kushindwa.Mfalme Albert wa Pili wa Ubelgiji amekubali ombi hilo la Leterme.

Vyama vya Ubelgiji vinapingana juu ya mageuzi kadhaa yenye lengo la kutowa madaraka zaidi kwa majimbo ya nchi hiyo.