BRUSSELS: Al-Qaeda tishio kubwa la ugaidi Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Al-Qaeda tishio kubwa la ugaidi Ulaya

Kiongozi mpya wa Umoja wa Ulaya kupiga vita ugaidi anasema,mtandao wa Al-Qaeda bado ni kitisho kikubwa cha ugaidi kwa nchi za umoja huo. Mbeligiji,Gilles de Kerchove amelionya Bunge la Ulaya kuhusu harakati za makundi ya Kiislamu kaskazini mwa Afrika.Amesema,mtandao wa al-Qaeda unayavutia makundi yenye itikadi kali kama vile Islamic Maghreb.

De Kerchove akaongezea kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kuchangamka zaidi,hasa katika upelelezi wa tovuti ili kuzuia makundi hayo kujiimarisha zaidi.Hapo awali idara ya upelelezi ya Uingereza MI5 ilisema,inaamini kuwa nchini humo kuna kiasi ya wakuruta 2,000 na miongoni mwao wapo watoto pia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com