1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brti Vogts kuwa kocha wa Nigeria ?

Ramadhan Ali15 Januari 2007

Aliekuwa kocha wa taifa wa Ujerumani,Berti Vogts huenda akatangazwa leo kocha mpya wa Nigeria.Kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati laingia nusu-finali huko Kigali.

https://p.dw.com/p/CHco

Roger Milla wa Kameroun achaguliwa ‚mwanasoka bora wa Afrika“ wa maiaka 50 iliopita na

Kombe la klabu bingwa za Afrika mashariki na kati laingia hatua ya nusu-fianli:

Werder Bremen yazingatia kumuajiri Mshambulizi wa Norway John Carew.

Viongozi wa shirikisho la dimba la Nigeria,walithibitisha jana kwamba wanazingatia wakati huu kumuajiri Berti Vogts kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani kuwa kocha mpya wa Super eagles.

Msemaji wa NFA-chama cha mpira cha Nigeria,Robin Okosun aliliambia shirika la habari la Ujerumani(DPA) mjini Abuja kuwa tangazo rasmi litatolewa leo.Kampuni moja la simu la Nigeria Globacom limejitolea kulipa shemu ya mshahara wa Berti Vogts.

Akithibitisha uwezekano wa kuwa kocha wa Nigeria, Vogts alisema hatahivyo kwamba hatazmii uamuzi wa haraka kupitishwa.Aliungama lakini kwamba amekutana na viongozi wa NFa kubadilishana fikra.Alisema zaidi kwamba, Nigeria ina timu nzuri ikiwa na wachezaji wengi stadi wa kibinafsi.

Berti vogts akiwa na umri wa miaka 60 hivi sasa aliichezea Ujerumani mara 96 kama beki-mshahara,akaibuka bingwa wa dunia na ujerumani 1974 na akawa kocha wa Ujerumani kati ya 1990 na 1998 na akaiongoza Ujerumani kutwa kombe la Ulaya la mataifa 1996.

Nae kocha mpya wa Ujerumani Joachim Loew amekanusha hofu kuwa timu yake ya taifa itadidimia chini na kushindwa kufikia matarajio makubwa yalioonekana mwaka jana-mwaka wa kombe la dunia nchini Ujerumani.

Ujerumani ilimaliza nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Itali na makamo-bingwa Ufaransa katika Kombe la dunia.Ujerumani inaanza mwaka mpya kwa dimba na Uswisi mwezi ujao mjini Dusseldorf-mojawapo ya changamoto 12 ilizopanga kwa mwaka huu.

Taarifa kutoka Lagos,Nigeria, zasema uchunguzi wa maoni uliofanywa na CAF-shirikisho la dimba la Afrika umebainisha kwamba Roger milla wa Kameroun, anaonekana ndie stadi bora kabisa wa dimba wa afrika alieibuka mnamo miaka 50 iliopita.

Taarifa iliotiwa saini na mkurugenzi wa CAF Suleiman Habuba, ilisema mzee Roger Milla aliecheza katika mashindano 3 mbali mbali ya kombe la dunia na simba wa nyika-Kameroun alijipatia kura 2246 na kumshinda stadi wa Misri Mahmoud El-Khatib aliejipatia kura 2165.

Roger Milla alitamba katika kombe la dunia 1982 nchini Spian,1990 nchini Itali na 1994 nchini Marekani.

Katika orodha ya wachezaji 10 bora kuna mastzadi kama Hossam Hassan(Misri),Samuel Eto’o (kameroun),Abedi Pele (Ghana),Gorge Weah (Liberia),Didier drigba (Ivory Coast), Nwanko Kanu (Nigeria),Rabah Madjer (Algeria) na Kalusha Bwalya (Zambia).

Labari kutoka Lome, zasema stadi wa Togo katika Kombe la dunia Emmanuel Adebayor alitishia jana kutoichezea tena timu ya taifa ya Togo mnamo miezi 6 ijayo.Sababu anatema, amevunjwa moyo na hali ya mpira katika timu ya Taifa iliokumbwa na mizozo kutoka mmoja hadi mwengine na hata kutia dosrai katika Kombe la dunia.

Kombe la klabu bingwa za Afrika mashariki na kati huko Kigali Ruanda-maarufu Kagame Cup-limemaliza jana duru za kwanza na katika msangao wa kwanza ni kufungishwa virago kwa Young Africans ya Tanzania na Vitalo ya Burundi na kurudishwa mzizima.

Revenue Authority ya Uganda ilivuna kweli jana kwani, iliizaba APR ya Randa mabao 3:0.

Kwa taarifa zaidi tujiunge sasa na muandishi wetu mjini Kigali, Christopher Karenzi akitufunulia kawa mambo yalivyopita: