1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brown atembelea vikosi vya Uingereza nchini Irak

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZWC

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefanya ziara ya ghafula kusini mwa Irak,kutembelea kituo cha kikosi cha Uingereza nje ya mji wa Basra. Amesema,vikosi vya Iraq vitakabidhiwa na Uingereza dhamana ya kulinda usalama baada ya kipindi cha kama majuma mawili yajayo.

Kabla ya ziara hiyo ya ghafula,Brown alitoa mwito wa kuachiliwa huru Waingereza 5 waliotekwa nyara nchini Irak.Ameyakataa madai ya watekanyara kuwa Uingereza iondoshe majeshi yake kutoka Irak.Hivi sasa Uingereza ina kama wanajeshi 4,500 nchini Irak.Idadi hiyo inatazamiwa kupunguzwa hadi 2,500 ifikapo kati kati ya mwaka ujao.