Brown atazamiwa kuongoza tofauti na Blair | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Brown atazamiwa kuongoza tofauti na Blair

Gordon Brown amepokea madaraka ya waziri mkuu wa Uingereza kutoka Tony Blair.Brown,aliekuwa waziri wa fedha,amekubali mualiko wa Malkia Elizabeth wa Pili,kuunda serikali mpya,baada ya kuwa na mkutano wa saa nzima katika kasri la Buckingham.

Gordon Brown

Gordon Brown

Baadae Brown akahamia makao rasmi ya waziri mkuu yalio Downing St. Namba 10.Alipowasili katika makao yake mapya,Brown aliwaambia waandishi wa habari kuwa atajitahidi kama awezavyo.Amesema, hiyo ni ahadi yake kwa watu wote wa Uingereza na sasa ndio ianze kazi ya mageuzi.

Waziri mkuu mpya Brown anatazamiwa kulitaja baraza lake la mawaziri baadae hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com