BRISBANE:Mshukiwa wa nane wa mashambulizi ya kigaidi akamatwa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRISBANE:Mshukiwa wa nane wa mashambulizi ya kigaidi akamatwa

Mshukiwa wanane kuhusika na majaribio ya mashambulizi ya kigaidi wiki iliyopita huko Scotland na London amekamatwa huko Australia.

Mshukiwa huyo daktari ambaye ni muhindi alikamatwa wakati alipokuwa akijaribu kusafiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Brisbane.

Maafisa wa Asutralia wanasema kuwa mtu alikuwa akifanyakazi katika hospitali moja jirani na Brisbane.

Hata hivyo waziri Mkuu wa Australia John Howard aliwatoa wasi wasi wananchi wake.

Nchini Uingereza, polisi wamekuwa wakiendelea upelelezi zaidi ambapo hali ya tahadhari ni ya kiwango cha juu.

Polisi wamesema kuwa wawili kati ya washukiwa saba waliyokamatwa mpaka sasa ni raia wa kutoka Jordan na Iraq wote wakiwa ni madaktari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com