1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRISBANE:Dr Haneef aachiwa kwa dhamana

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiE

Daktari mmoja aliyeshtakiwa kwa kuhusika katika jaribio la shambulio la bomu katika miji ya London na Glasgow nchini Uingereza ameachiwa kwa dhamana.Mohamed Haneef aliye na umri wa miaka 27 ni daktari aliye na asili ya kIhindi aliyehamia nchini Australia mwaka jana akitokea nchini Uingereza.Kwa mujibu wa duru za polisi daktari huyo anadaiwa kuwa aliwapa washukiwa wawili wa shambulio hilo kadi yake ya simu.Haneef alishtakiwa siku ya jumamosi na kuomba kuachiwa kwa dhamana hii leo.Kulingana na polisi hatua ya kuwaazima washukiwa hao kadi yake simu ilikuwa uzembe wala sio makusudi.Wakili wa daktari huyo anasema kuwa kesi hiyo haina ushahidi wa kutosha.Jaji Jacqui Payne alimruhusu Dr Haneef kuachiwa kwa dhamana ya euro alfu 6300,kutoa ripoti kwa polisi kwa polisi mara tatu kwa wiki aidha kutofika kwenye kiwanja chochote cha ndege cha kimataifa.Daktari huyo amekabidhi polisi hati yake ya kusafiria huku akisubiri kutoa dhamana aliyoruhusiwa.