1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bremen na Gladbach zaduwazwa

5 Agosti 2013

Msimu mpya wa ligi ya soka Ujerumani umeng'oa nanga mwishoni mwa juma kwa mechi za duru ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Ujerumani na kama kawaida dimba hilo halikukosa mshangao

https://p.dw.com/p/19KAg
DARMSTADT, GERMANY - AUGUST 04: Christoph Kramer of Moenchengladbach is challenged by Marco Sailer of Darmstadt during the DFB Cup first round match between Darmstadt 98 and Borussia Moenchengladbach at Boellenfalltorstadion on August 4, 2013 in Darmstadt, Germany. (Photo by Alex Grimm/Bongarts/Getty Images)
Fußball - DFB Cup Darmstadt 98 - Borussia MoenchengladbachPicha: Getty Images

Werder Bremen na Borussia Moenchengladbach walikuwa waathiriwa wa kwanza wa Bundesliga kubanduliwa nje ya kombe hilo kufikia sasa na timu za ligi ya daraja ya tatu.

Timu nyingine mbili za Bundesliga zilitolewa wakatin klabu iliyopandishwa msimu huu Eintracht Braunschweig ilipofungwa magoli mawili kwa moja na timu ya daraja ya pili Arminia Bielefeld, nayo Nuremberg ikashindwa kupitia mikwaju ya penalty mabao matano kwa manne na klabu ya daraja ya pili Sandhausen.

Kocha Robin Dutt wa Werder Bremen hakuamini macho yake
Kocha Robin Dutt wa Werder Bremen hakuamini macho yake baada ya kuzidiwa nguvuPicha: Getty Images

Bremen walitemwa nje kwa kufungwa mabao matatu wka moja katika muda wa nyongeza na klabu ya Saarbrücken ikiwa ni mara yao ya tatu mfululizo kuondolewa katika dimba hilo kwenye duru ya kwanza na timu ya ligi xya daraja ya tatu. Huo ulikuwa mwanzo mbaya wa ligi kwa kocha mpya Robin Dutt aliyechukua mikoba kutoka kwa Thomas Schaaf. Nao Gladbach walimaliza mchezo bila kufungana na Darmstadt katika muda wa ziada na wakanyolewa kwa penalti kwa kufungwa mabao matano kwa manne.

Timu nyingine zilizofuzu kwa awamu ijayo ni Hanover, Eintracht Frankfurt, SV Hamburg pamoja na Borussia Dortmund. Hii leo itakuwa zamu ya Bayern Munich na Schalke ambazo zitaingia uwanjani dhidi ya wapinzani wa daraja ya chini.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman