1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yaahidi usalama wakati wa Olimpiki

11 Machi 2016

Maafisa nchini Brazil wamepuuza vitisho vya kuzuka maandamano makubwa wakati wa michezo ya Olimpiki, licha ya mgogoro wa uchmi na kisiasa na sakata linalochipuka la ufisadi katika kampuni ya serikali ya mafuta, Petrobas

https://p.dw.com/p/1IBt1
Brasilien Unruhen
Picha: CHRISTOPHE SIMON/AFP/Getty Images

Waziri wa UIinzi wa Brazil Aldo Rebelo anasema anatarajia kuwa maafisa wa usalama 85,000, wakiwemo wanajeshi 38,000 watatosha kuhakikisha usalama wakati wa mashindano hayo ya Rio de Janeiro kuanzia Agosti tano hadi 21. "kuhusiana na uwezekano wa ikiwa kutakuwa au hakutakuwa na maandamano ya umma, nadhani hayakutakuwapo. Sidhani kama tutashuhudia maandamano kama ya 2013 na kidogo mwanzoni mwa Kombe la Dunia 2014 kwa sababu wakati wa Kombe la Dunia 2014 hofu ilitulizwa sana. Nadhani Olimpiki itakuwa na mazingira tulivu zaidi ukilinganisha na 2013".

Baadhi ya makundi ya wakaazi wa Rio de Janeiro wameahidi kuandamana tena wakati wa michezo hiyo, hasa yale yanayowawakilisha watu walioachwa bila makaazi kutokana na miradi ya ujenzi kwa ajili ya Olimpiki.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Gakuba Daniel