1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil na Uholanzi kupambana robofainali

29 Juni 2010

Katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko Afrika Kusini, jana usiku Brazil ilifanikiwa kuingia robofainali baada ya kuichabanga Chile mabao 3-0.

https://p.dw.com/p/O5NA
Kikosi cha BrazilPicha: AP

Brazil sasa itapambana Uholanzi ambayo hapo jana iliifunga Slovakia mabao 2-1.

Yalikuwa ni mabao ya Juan, Luis Fabiano na Robinho yaliyoipatia ushindi huo Brazil, timu inayopigiwa upatu mkubwa kutwaa kombe hilo.

WM 2010 Südafrika Achtelfinale - Brasilien gegen Chile Flash-Galerie
Luis Fabiano akipachika bao la pili la Brazil dhidi ya ChilePicha: AP

Timu nyingine zilizofanikiwa kuingia robofainali ni pamoja na Ujerumani iliyosambaratisha Uingereza mabao 4-1 na sasa itapambana na Argentina hapo siku ya Jumamosi.

Ghana ambayo ndiyo timu pekee kutoka Afrika iliyosalia itaingia dimbani katika robofainali hapo siku ya Ijumaa kwa kupambana na Uruguay.Leo hii Paraguay inacheza na Japan, kabla ya Uhispania kucheza na Ureno.

Mwandishi:Aboubakary Liongo