1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brassels.Alioyekuwa amefungwa Guantanamo Bay ailaumu Ujerumani na Uturuki.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq4

Raia wa Uturuki aliyezaliwa Ujerumani amewalaumu maafisa wa Ujerumani na Uturuki kwa kushindwa kumsaidia kufuatia miaka yake mitano ya kifungo katika jela ya Kijeshi ya Kimarekani ya Guantanamo Bay iliyopo nchini Cuba.

Murat Kurnaz aliyeachiliwa huru mwezi August, ameiambia kamati maalum ya Bunge la Ulaya iliyokutana Brussels kwamba, si Berlin wala Ankara iliyojishughulisha kumtoa katika kifungo huko Guantanamo.

Aidha amewalaumu wanajeshi wa jeshi maalum la Ujerumani kwa kumtendea vibaya nchini Afghanistan kabla hajahamishiwa Guantanamo Bay.